2 Mose 7 - Swahili Roehl Bible 1937

Mose na Haroni wanafanya vielekezo machoni pake Farao.

1Kisha Bwana akamwambia Mose: Tazama, nimekupa kuwa kama Mungu kwake Farao, naye kaka yako Haroni atakuwa mfumbuaji wako.Pigo la kwanza: Maji yanageuka kuwa damu.

14Bwana akamwambia Mose: Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwapa watu hawa ruhusa kwenda zao.

15Kesho asubuhi nenda kwa Farao, utakapomwona, akitoka kwenda majini! Nawe simama hapo ukingoni kwa mto na kumngoja ukiishika mkononi mwako ile fimbo iliyogeuka kuwa nyoka!

16Nawe umwambie: Bwana Mungu wa Waebureo amenituma kwako kukuambia: Hao watu walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie nyikani! Lakini mpaka hapa hujasikia bado.2 Mose 5:1.

17Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa hili na utambue, ya kuwa mimi ni Bwana: Tazama! Mimi nitakapoyapiga maji yaliyomo humu mtoni kwa fimbo hii, ninayoishika mkononi, ndipo, yatakapogeuka kuwa damu.2 Mose 4:9.

18Nao samaki waliomo humu mtoni watakufa, nao mto utanuka vibaya, nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni.

19Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Ichukue fimbo yako, kisha ukunjue mkono wako na kuuelekezea maji yao ya Misri yaliyomo vijitoni namo majitoni namo maziwani namo mashimoni, maji yanamokusanyika, yageuke kuwa damu! ndipo, yatakapogeuka kuwa damu katika nchi yote nzima ya Misri, nayo yaliyomo katika vyombo vya miti namo katika vyombo vya mawe.Ufu. 11:6.

20Mose na Haroni wakafanya hivyo, kama Bwana alivyoagiza. Haroni alipoinyanyua hiyo fimbo na kuyapiga maji yaliyomo humo mtoni machoni pake Farao napo machoni pao watumishi wake, ndipo, maji yote yaliyomo humo mtoni yalipogeuzwa kuwa damu.

21Nao samaki waliokuwamo mtoni wakafa, nao mto ukanuka vibaya, Wamisri wasiweze kuyanywa hayo maji ya mtoni, maana yote yaligeuka kuwa damu katika nchi nzima ya Misri.

22Lakini waganga wa Misri wakavifanya nao kwa uganga wao; ndipo, moyo wake Farao uliposhupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.2 Mose 7:11.

23Kisha Farao akageuka, akaingia nyumbani mwake, pasipo kuviweka moyoni mwake.

24Wamisri wote wakachimba maji pande zote za mtoni, wapate ya kunywa, kwani maji ya mtoni hawakuweza kuyanywa.

25Vikawa hivyo siku saba zote, Bwana alipokwisha kuupiga huo mto.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help