1Neno la Bwana likanijia la kwamba:Ufunuo wa maangamizo ya Sidoni.
20Neno la Bwana likanijia la kwamba:
21Mwana wa mtu, uuelekezee Sidoni uso wako na kuufumbulia yatakayokuwa!Yes. 23:2,12.
22Sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia, Sidoni, nijitokeze katikati yako kuwa mtukufu. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapouhukumu, nijulike mwake, ya kuwa ni mtakatifu.2 Mose 14:18.
23Nitatuma kwake magonjwa mabaya na damu barabarani mwake, waangushwe mwake chini po pote waliopigwa kwa panga; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
24Mlango wa Isiraeli hautaona tena miiba ya kuwachoma wala machomo ya kuwaumiza kwao wote wanaokaa na kuwazunguka waliowabeza; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
Wokovu wa Isiraeli.25Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitakapowakusanya walio ukoo wa Isiraeli na kuwatoa kwenye makabila yote, walikotawanyikia, ndipo, nitakapoutokeza kwao utakatifu wangu, wao wa mataifa wauone; nao watakaa katika nchi yao, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
26Nao watakaa huko kwa kutulia, wajenge nyumba, wapande mizabibu; watakaa kwa kutulia, kwa kuwa nitawakatia mashauri kwao wote wanaokaa na kuwazunguka waliowabeza. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu wao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.