Yesaya 37 - Swahili Roehl Bible 1937

Hizikia anaomba wokovu kwa Bwana na kuupata.(1-38: 2 Fal. 19:1-37.)

1Ikawa, mfalme Hizikia alipoyasikia, akazirarua nguo zake, akajifunga gunia, akaingia Nyumbani mwa Bwana.

21Ndipo, Yesaya, mwana wa Amosi, alipotuma kwake Hizikia kumwambia: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Isiraeli, uliyemlalamikia kwa ajili ya Saniheribu, mfalme wa Asuri.

22Hili ndilo neno, Bwana alilolisema kwa ajili yake: Mwanamwali binti Sioni, amekubeza na kukufyoza; binti Yerusalemu, amekutingishia kichwa nyuma yako.

23Ni nani, uliyembeua na kumtukana? Ni nani, uliyempalizia sauti na kuyaelekeza macho yako juu? Ni Mtakatifu wa Isiraeli.

24Bwana ndiye, uliyembeua vinywani mwa watumishi wako ukisema: Kwa kuwa magari yangu ni mengi, nimepanda milimani juu huko ndani Libanoni, nikaikata miangati yake mirefu na mivinje yake iliyochaguliwa, nikafika kwake huko juu kileleni, msitu unakokuwa kama shamba lake la miti.

30Hiki kitakuwa kielekezo chako, Hizikia: Mwaka huu mtakula yaliyojipanda yenyewe, mwaka wa pili mtakula yaliyoota mashinani, mwaka wa tatu mmwage mbegu, mvune. Nayo mizabibu mtapanda, myale matunda yao.

31Ndipo, masao yao waliopona wa mlango wa Yuda watakapotia mizizi chini, kisha watazaa matunda juu.Yes. 27:6.

32Kwani Yerusalemu yatatokea masao, nako mlimani kwa Sioni watatokea waliopona. Wivu wake Bwana Mwenye vikosi utayafanya hayo.

33Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya mfalme wa Asuri: Hatauingia mji huu, wala hatapiga humu mshale, wala hataukaribishia ngao, wala hataujengea boma la kuuzingia.

34Njia, aliyokuja nayo, ileile atarudi nayo. Lakini humu mjini hatamwingia; ndiyo, asemavyo Bwana.

35Nitaukingia mji huu, niuokoe kwa ajili yangu mimi na kwa ajili ya mtumishi wangu Dawidi.

36Akatokea malaika wa Bwana, akapiga makambini kwa Waasuri watu 185000. Walipoamka asubuhi wakawaona hao wote, ya kuwa wamekufa, ni mizoga tu.Yes. 17:14; 31:8.

37Ndipo, Saniheribu, mfalme wa Asuri, alipoondoka, aende zake, akarudi kwao, akakaa Niniwe.

38Ikawa, alipoomba nyumbani mwa mungu wake Nisiroki, ndipo, wanawe, Adarameleki na Sareseri walipompiga kwa upanga, ksha wakaikimbilia nchi ya Ararati, naye mwanawe Esari-Hadoni akawa mfalme mahali pake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help