1Wamwegemeao Bwana hufanana nao mlima wa Sioni, hautikisiki, unakaa kale na kale.
2Kama milima inavyouzunguka mji wa Yerusalemu, ndivyo, Bwana anavyowazunguka walio ukoo wake kuanzia sasa hata kale na kale.
3Kwani bakora yao wasiomcha Mungu haitashika uflame wa kulitawala fungu lao walio waongofu, kusudi waongofu wasiipeleke mikono yao kushika yenye mapotovu.
4Bwana, walio wema wafanyizie mema, nao wanyokao mioyo!
5Lakini wao wazigeuzao njia zao kuwa za kuptokapotoka Bwana an awaache, wajiendee pamoja nao wafanyao maovu! Utengemano na uwakalie wao Waisiraeli!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.