Matendo ya Mitume 22 - Swahili Roehl Bible 1937

Paulo anasema na watu.

1Waume mlio ndugu na baba, sikilizeni, ninayojikania sasa mbele yenu!(3-21: Tume. 9:1-29; 26:9-20.)

3Akasema: Mimi ni mtu wa Kiyuda, nimezaliwa Tarso katika nchi ya Kilikia. Nikalelewa humu mjini, nikakaa miguuni pa Gamalieli na kufundishwa Maonyo ya baba zetu kwa uangalifu wote. Nikajipingia kumfanyia Mungu kazi, kama nanyi nyote leo.

22Ndipo, wale waliomsikiliza mpaka neno hili walipopaza sauti wakisema: Mwondoe huyu nchini! Kwani haimpasi kuwapo.Tume. 21:36.

23Walipopiga kelele hivyo na kuzirarua nguo zao na kutupa uvumbi juu angani,

24mkuu wa kikosi akaagiza, aingizwe bomani; akasema, wamwulize kwa mapigo, apate kuijua sababu ya kumpigia makelele kama hayo.

25Walipomfunga kwa mikanda, apigwe, Paulo akamwambia bwana askari aliyesimama hapo: Je? Mko na ruhusa kupiga mtu aliye Mroma, asipohukumiwa kwanza?Tume. 16:37-38; 23:27.

26Bwana askari alipovisikia hivi akamwendea mkuu wa kikosi, akamjulisha akisema: Wataka kufanya nini? Kwani mtu huyu ni Mroma.

27Mkuu wa kikosi akamwendea, akamwambia: Niambie, wewe u Mroma? Naye akasema: Ndio.

28Mkuu wa kikosi alipojibu: Mimi huu Uroma nimeununua kwa fedha nyingi, Paulo akasema: Mimi nimezaliwa nao.

29Papo hapo wale waliotaka kumwuliza kwa mapigo wakamwacha. Naye mkuu wa kikosi akaogopa alipotambua, ya kuwa ni Mroma, kwani yeye alimfunga.

Paulo mbele ya wakuu.

30Kesho yake alitaka kuyatambua mashtaka ya Wayuda, kama ni ya kweli; kwa hiyo akamfungua, akaagiza, watambikaji wakuu na baraza yote ya wakuu wakusanyike pamoja, akampeleka Paulo chini kwao, akamsimamisha mbele yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help