1*Neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana ni hili:
2Simama langoni mwa Nyumba ya Bwana, ulitangaze neno hili huko ukisema: Lisikieni neno la Bwana, ninyi Wayuda wote mnaoingia humu malangoni kumwangukia Bwana!
3Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli: Ziangalieni njia zenu na matendo yenu, yawe mema! Ndipo, nitakapowakalisha katika nchi hii.
12Haya! Nendeni mahali pangu kule Silo, nilipolikalisha Jina langu kwanza, myaone yote, niliyopafanyizia kwa ajili ya ubaya wao Waisiraeli walio ukoo wangu!Kutambikia vinyago huleta mapatilizo.
29Binti Sioni, zinyoe nywele zako za urembo, uzitupe! Piga kilio vilimani juu kusikokuwa na vijiti! Kwani Bwana amekikataa kizazi kilichomkasirisha, akakitupa.
30Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Wana wa Yuda wamefanya yaliyo mabaya machoni pangu, wakaweka matapisho yao katika Nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, waichafue.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.