1Siku ile Debora na Baraka, mwana wa Abinoamu, wakaimba kwamba:
2Kwa kuwa walikuwako waliowaongoza Waisiraeli, kwa kuwa nao watu wamejitoa wenyewe, kwa hiyo mtukuzeni aliye Bwana!
3Sikieni, ninyi wafalme! Sikilizeni, ninyi watawalaji! Mimi, mimi mwenyewe na nimwimbie Bwana, na nimshangilie Bwana Mungu wa Isiraeli!
4Bwana, ulipotoka Seiri, ulipopita mashambani kwa Edomu, nchi ikatetemeka, mbingu nazo zikanyesha, mawingu nayo yakanyesha mvua.
6Siku za Samugari, mwana wa Anati, barabara zilikuwa zimekufa, hata siku za Yaeli; nao walioshika njia hupitia zile za kupotokapotoka.
9Moyo wangu huwaelekea waongozi wa Waisiraeli waliojitoa wenyewe miongoni mwa watu. Mtukuzeni aliye Bwana!
10Ninyi mpandao punda weupe, nanyi mkaliao mazulia, nanyi mtembeao njiani: yafikirini mioyoni!
Kisha nchi ikapata kutulia miaka 40.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.