Mpiga mbiu 8 - Swahili Roehl Bible 1937

Wanaotii ukuu nao wamchao Mungu hupata mema.

1Aliye kama mwerevu wa kweli ni nani? Tena yuko nani ajuaye maana ya mambo? Werevu wa kweli wa mtu huuangaza uso wake, ushupavu wa uso wake ugeuzwe.

2Mimi husema: Kiangalie kinywa cha mfalme, kwa kuwa uliapa na kumtaja Mungu!

3Usitoke upesi usoni pake, wala usishikamane na shauri baya! Kwani yeye hufanya yote yampendezayo.

4Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu, yuko nani awezaye kumwambia: Unafanya nini?

5Aishikaye amri yake hataona baya lo lote; nao moyo wa mwerevu wa kweli hujua, siku za wakati wa kukatia shauri zitakapotimia.

6Kwani kila jambo liko na siku zake za kukatiwa shauri. Kwani huu ndio ubaya unaowalemea watu sana:

16Mara kwa mara nikauelekeza moyo wangu, uujue werevu wa kweli kwa kuzitazama kazi za utumishi zinazofanywa huku nchini, kwani wako wasioona usingizi machoni pao mchana wala usiku.

17Ndipo, nilipozitazama kazi zote za Mungu, nikaona, ya kuwa mtu hawezi kuzitambua maana hizo kazi zinazofanywa chini ya jua; ijapo mtu ajisumbue sana kwa kuitafuta hiyo maana, haioni. Hata mwerevu wa kweli akijiwazia kwamba ameijua, hawezi kuitambua.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help