Mifano 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Kualika watu, waje kuerevuka.Mifano ya Salomo, mwana wa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli.

1Waje kujua werevu wa kweli na kuonyeka,

2wajue kutambua maneno ya utambuzi,

3waje kuonyeka, wapate akili,

tena wapate wongofu na mashauri mema yaongokayo,

4waerevushe wajinga,

nao wavulana wawajulishe kuwaza mambo mioyoni!

5Naye mwerevu wa kweli ayasikie, auongeze ujuzi wake,

naye mtambuzi ajipatie wongozi mwema.

6atambue mifano na vitendawili,

hata maneno ya werevu wa kweli na mafumbo yao!

7Kumcha Bwana ndio mwanzo wa ujuzi,

lakini wajinga huubeza werevu wa kweli kwa kukataa kuonyeka.

8Mwanangu, sikia, baba yako akikuchapa,

usiyabeue maonyo ya mama yako!Kuonya watu, wasidanganyike.

10Mwanangu wakosaji wakikubembeleza, usiwaitikie!

11Wakikuambia: Twende pamoja, tuvizie kumwaga damu,

tena tumwotee bure asiyekosa,

12kama kuzimu tuwameze, wakingali wa hai,

wao wamchao Mungu wawe kama wengine washukao shimoni,

13tuzipate mali zao zote zenye kima,

tuzijaze nyumba zetu mateka,

14kisha nawe utapiga kura pamoja nasi,

sisi sote pia tutakuwa bia moja tu:

15mwanangu, hao usishike njia moja nao,

uzuie mguu wako, usikanyage mikondo yao!

16Kwani miguu yao hukimbilia mabaya,

hupiga mbio kuja kumwaga damu.

17Ni bure, wavu ukiwa umetandwa

machoni pao wote walio wenye mabawa.

18Hivyo wao huvizia kumwaga damu zao wenyewe

na kuziotea roho zao wenyewe.

19Ndivyo, zilivyo njia zao wote wanaotamani mali tu,

maana giza huzichukua roho zao wenyewe.

Mapatilizo yao wasiosikia.

20Werevu wa kweli hupiga mbiu barabarani,

huipaza sauti yake viwanjani;

21hutangaza pembeni penye njia pasipo na makelele mengi,

napo pa kuingia malangoni, namo mjini husema maneno yake:

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help