1*Katika mwanzo wa ufalme wa Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, ndipo, neno hili lilipotoka kwake Bwana kwamba:
2Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Simama uani pa Nyumba ya Bwana, nao watu wa miji yote watakaopaingia kutambika Nyumbani mwa Bwana uwaambie maneno yote, niliyokuagiza kuwaambia, usipunguze hata neno moja.
3Labda watasikia, warudi kila mmoja katika njia yake mbaya, nipate kugeuza moyo kwa ajili ya mabaya, niliyoyawaza kuwafanyizia kwa matendo yao mabaya.Mfumbuaji Uria anauawa.
20Kulikuwa na mtu mwingine aliyefumbua katika Jina la Bwana, ni Uria, mwana wa Semaya wa mji wa Kiriati-Yearimu. Naye akayafumbua yote yatakayoujia mji huu na nchi hii sawasawa kama Yeremia.
21Mfalme Yoyakimu na watu wake wote wa vita na wakuu wote walipoyasikia maneno yake, mfalme akatafuta, jinsi atakavyomwua. Uria alipoyasikia, akaogopa, akakimbia kwenda Misri.
22Mfalme Yoyakimu akatuma watu kwenda Misri; ni Elnatani, mwana wa Akibori, na watu wengine waliokwenda naye Misri.
23Wakamtoa Uria huko Misri, wakampeleka kwake mfalme Yoyakimu, akampiga kwa upanga, mzoga wake akautupa kwenye makaburi yao waliokuwa wa ukoo huu.
24Lakini Ahikamu, mwana wa Safani, alimshika Yeremia kwa mkono wake, asitiwe mikononi mwa watu wamwue.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.