1Bwana akamwambia Mose kwamba:
2Kila mtoto mume atakayezaliwa wa kwanza na mama yake ye yote, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga kwao wana wa Isiraeli, sharti amtoe kuwa wangu mimi. Kwani ni wangu kweli.Agizo la kula mikate isiyochachwa.
3Mose akawaambia hao watu: Ikumbukeni siku hii ya leo kuwa ndiyo, mliyotoka huko Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa! Kwani Bwana amewatoa huko kwa mkono wenye uwezo, siku hiyo kisiliwe cho chote chenye chachu.
4Siku hii ndiyo, mliyotoka nayo katika mwezi wa Abibu.
20Walipoondoka Sukoti wakapiga makambi Etamu kwenye mpaka wa hiyo nyika.
21Naye Bwana akawaongoza akiwatangulia mchana kwa wingu jeusi lililokuwa kama nguzo, awaongoze njia, tena usiku kwa moto uliokuwa kama nguzo, uwamulikie, wapate kwenda mchana na usiku.2 Mose 40:34; 4 Mose 9:15-23; 1 Kor. 10:1.
22Ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana mbele yao hao watu, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku mbele yao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.