1Siku hiyo, watu waliposomewa masikioni pao yaliyoandikwa katika kitabu cha Maonyo, pakaoneka palipoandikwa kwamba: Kale na kale asije Mwamoni wala Mmoabu kuuingia mkutano wa Mungu!
10Nikajulishwa, ya kuwa Walawi hawakupewa mafungu yao yawapasayo; kwa hiyo Walawi na waimbaji waliofanya kazi za Mungu walikuwa wamekimbilia kila mtu shamba lake.
11Ndipo, nilipowagombeza watawalaji na kuwauliza: Mbona Nyumba ya Mungu imeachwa hivyo? Nikawakusanya, nikawaweka tena mahali pao pa utumishi.
15Siku hizo nikaona katika nchi ya Yuda, ya kuwa wako wanaokanyaga makamulio siku ya mapumziko, ya kuwa wengine hupeleka machungu ya ngano chanjani kwa kuchukuza punda, wakawatwika hata mvinyo, zabibu, kuyu na mizigo yo yote, wakaipeleka Yerusalemu siku ya mapumziko. Ndipo, nilipowaonya hiyo siku, walipouza vilaji.
23Tena nikaona siku hizo, ya kuwa wako Wayuda waliooa wake wa Waasdodi na wa Waamoni na wa Wamoabu.
24Nao wana wao nusu wakasema Kiasdodi, hawakuweza kusema Kiyuda, ila walisema misemo yao hawa na hawa.
25Nikawagombeza na kuwaapiza na kuwapiga, waume wengine nikawavuta nywele. Kisha nikawaapisha na kumtaja Mungu kwamba: Msiwaoze wana wao wana wenu wa kike, wala msichukue kwao wana wa kike, mwape wana wenu wa kiume au mwaoe wenyewe!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.