3 Mose 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Mambo mengine ya ng'ombe za tambiko za weuo.

1Tena mtu anaweza kukosa hivi: akisikia shaurini sauti ya mwenye kuapiza, naye ni shahidi kwa kuliona lile jambo au kwa kulijua, basi, asipolieleza, atakuwa amekora manza zitakazomkalia.

11Lakini mkono wake usipowafikilia hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga, basi, toleo lake, atakalopeleka, kwa kuwa alikosa, na liwe vibaba viwili na nusu vya unga mwembamba kuwa kipaji chake cha tambiko cha weuo; asiumiminie mafuta, wala asitie uvumba juu yake, kwani ndio kipaji cha tambiko cha weuo.Maagizo ya ng'ombe za tambiko za upozi.

14Bwana akamwambia Mose kwamba:

15Mtu akilivunja Agano, akikosa kwa kuchukua kitu kilicho mali ya Bwana, asipovijua, na ampelekee Bwana ng'ombe yake ya tambiko ya upozi, akitoa katika kundi lake dume la kondoo asiye na kilema, unayemwona kuwa wa fedha mbili tatu zilizopimwa kwa kipimo cha Patakatifu; huyo atakuwa ng'ombe yake ya tambiko ya upozi.

16Kisha nazo mali za Patakatifu, alizozikosea kwa kuzichukua, atazilipa na kuongeza fungu la tano; zote ampe mtambikaji. Ndipo, mtambikaji atakapompatia upozi na kumtoa yule dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi, kisha ataondolewa kosa lake.

17Hata mtu akikosea agizo lo lote la Bwana, ijapo ni moja tu, kwa kufanya yasiyofanywa, asipovijua, naye atakuwa amekora manza, nao uovu wake utamkalia.

18Kwa hiyo na atoe katika kundi lake dume la kondoo asiye na kilema, unayemwona, ya kama anatosha kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi. Kisha ampeleke kwa mtambikaji, naye mtambikaji atampatia upozi kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa pasipo kulijua kuwa ni kosa; naye akiwa hakuvijua kweli ataondolewa kosa lake.

19Basi, hii ni ng'ombe ya tambiko ya upozi, kwa maana manza, alizozikora, alizikora kwake Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help