1Ahazi alikuwa mwenye miaka 20 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 16 mle Yerusalemu; hakuyafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama baba yake Dawidi,
2ila akaendelea kuzishika njia za wafalme wa Waisiraeli, akatengeneza navyo vinyago vya Mabaali vilivyoyeyushwa.
3Naye yeye akavukiza bondone kwa Bin-Hinomu, hata wanawe akawatumia kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa motoni akiyafuata hayo matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli.Mungu anampatiliza Ahazi.
16Siku zile mfalme Ahazi akatuma kwao wafalme wa Asuri, waje kumsaidia,
17kwa maana Waedomu walikuja tena, wakawapiga, wakachukua mateka.
18Nao Wafilisti wakaiingia miji ya nchi ya tambarare na miji ya kusini katika nchi ya Yuda na kunyang'anya mali, wakateka Beti-Semesi na Ayaloni na Gederoti na Soko na mitaa yake na Timuna na mitaa yake na Gimuzo na mitaa yake, wakakaa humo.
19Kwani Bwana aliwanyenyekeza Wayuda kwa ajili ya Ahazi, mfalme wa Waisiraeli, kwani aliwalegeza Wayuda alipomvunjia Bwana maagano.
20Ndipo, Tilgati-Pilneseri, mfalme wa Asuri, alipomjia, lakini akamsonga, hakumpatia nguvu.
21Kwani Ahazi alichukua kwa nguvu yaliyokuwamo Nyumbani mwa Bwana namo nyumbani mwa mfalme nazo mali za wakuu, akampa mfalme wa Asuri, lakini hakusaidiwa naye.
22Papo hapo, aliposongeka, yeye mfalme Ahazi akazidi kumvunjia Bwana maagano,
23akaitumikia miungu ya Damasko iliyompiga, akasema: kwa kuwa miungu ya wafalme wa Ushami ndiyo iliyowasaidia, basi, nitaitambikia hiyohiyo, wanisadie; nayo ndiyo iliyomkwaza mwenyewe na Waisiraeli wote.
24Kisha Ahazi akavikusanya vyombo vya Nyumba ya Mungu, akavivunjavunja hivyo vyombo vya Nyumba ya Mungu, akaifunga milango ya Nyumba ya Bwana, akajitengenezea pa kutambikia pembeni po pote mle Yerusalemu.
25Hata kila mji mmoja wa Yuda akautengenezea vilima vya kuvukizia miungu mingine juu yao; ndivyo, alivyomkasirisha Bwana Mungu wa baba zake.
Kufa kwake Ahazi.26Mambo yake mengine na njia zake zote, za kwanza na za mwisho, tunaziona, zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Wayuda na wa Waisiraeli.
27Kisha Ahazi akaja kulala na baba zake, wakamzika katika mji wa Yerusalemu, kwani hawakumpeleka penye makaburi ya wafalme wa Waisraeli. Naye mwanawe Hizikia akawa mfalme mahali pake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.