1Katika siku za Dawidi kulikuwa na njaa mwaka kwa mwaka, miaka mitatu; naye Dawidi alipoutafuta uso wa Bwana, Bwana akasema: Ziko manza za damu, Sauli nao wa mlango wake walizozikora walipowaua watu wa Gibeoni.
2Ndipo, mfalme alipowaita Wagibeoni kusema nao; nao Wagibeoni hawakuwa wana wa Isiraeli, ila walikuwa masao yao Waamori, nao wana wa Isiraeli walikuwa wamefanya maagano nao na kuapa, lakini Sauli alitaka kuwaua kwa kuona wivu kwa ajili ya wana wa Isiraeli na wa Yuda.Wafilisti wanashindwa.
15Baadaye Wafilisti walipokuja tena kupigana na Waisiraeli, Dawidi akashuka pamoja na watumishi wake. Walipopigana na Wafilisti, Dawidi akachoka.
16Ndipo, alipotokea Isibi-Benobu aliyekuwa mmoja wao yale Majitu marefu; huyu alikuwa na mkuki wenye ncha ya shaba, nayo ilipopimwa, uzito wake ulikuwa sekeli 300, ndio nusu ya frasila; naye alikuwa amejifunga mata mapya, akataka kumwua Dawidi.
17Ndipo, Abisai, mwana wa Seruya, alipomsaidia na kumpiga yule Mfilisti, hata akafa. Hapo ndipo, watumishi wa Dawidi walipomwapia kwamba: Wewe hutatoka tena pamoja na sisi kwenda vitani, usiizime taa ya waisiraeli!(18-22: 1 Mambo 20:4-8.)
18Hayo yalipokwisha yakawa mapigano mengine nao Wafilisti kule Gobu; ndiko, Sibekai wa Husa alikomwua Safu aliyekuwa naye mmoja wao yale Majitu marefu.
19Kisha kule Gobu yakawa mapigano mengine na Wafilisti; ndiko, Elihanani wa Beti-Lehemu, mwana wa Yare-Orgimu, alikomwua Goliati wa Gati; huyu uti wa mkuki wake ulikuwa kama majiti ya wafuma nguo.1 Sam. 17:7.
20Kisha yakawa mapigano tena kule Gati; huko kulikuwa na mtu mrefu sana, vidole vya mikono yake na vidole vya miguu yake vilikuwa sita sita, vyote pamoja ni 24, naye alikuwa amezaliwa kwao yale Majitu marefu.
21Alipowatukana Waisiraeli, Yonatani, mwana wa Simea, kaka yake Dawidi, akamwua.1 Sam. 17:10.
22Hawa wanne walizaliwa Gati kwao yale Majitu marefu, wakauawa kwa mikono ya Dawidi na kwa mikono ya watumishi wake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.