Yeremia 18 - Swahili Roehl Bible 1937

Mfano wa mfinyanzi.

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwake Bwana kwamba:

2Inuka, ushuke kwenda nyumbani mwa mfinyanzi. Ndimo, nitakamokuambia maneno yangu.

3Nikashuka kwenda nyumbani mwa mfinyanzi, nikamkuta, akifanya kazi kwenye kibao chake.

4Chombo, mfinyanzi alichokifanya na mkono wake, kisipokuwa chema, basi, akakitengeneza kuwa chombo kingine, kama ilivyofaa machoni pake mfinyanzi kukifanya.

5Neno lake Bwana likanijia kwamba:

6Kama huyu mfinyanzi nami siwezi kuwafanyizia ninyi mlio mlango wa Isiraeli? ndivyo, asemavyo Bwana. Tazameni: kama udongo ulivyo mkononi mwa mfinyanzi. ndivyo, ninyi mlio mlango wa Isiraeli mlivyo mkononi mwangu.Njama ya kumwua Yeremia na kuomba kwake.

18Wakasema: Njoni, tumlie Yeremia njama ya kumwazia mawazo! Kwani maonyo hayampotelei mtambikaji, wala mizungu haimpotelei mjanja, wala maneno hayampotelei mfumbuaji. Haya! Tumpige tukiyatumia, ulimi wake uliyoyasema! Tusiyasikilize maneno yake yote!

19Bwana, nisikilize! Isikie sauti ya wapingani wangu!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help