1Bwana akamwambia Mose kwamba:Ng'ombe za tambiko za sikukuu ya Pasaka.
16Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza ni Pasaka ya Bwana.3 Mose 23:5-14.
17Siku ya kumi na tano ya mwezi huo na mle sikukuu; ndipo iliwe mikate isiyochachwa siku saba.
18Siku ya kwanza na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi,4 Mose 28:25-26.
19ila mmtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima motoni: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema; hawa ndio, mtakaowatoa.
20Navyo vilaji vyao vya tambiko na mtoe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya dume la kondoo.4 Mose 28:12.
21Tena na mtoe vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
22Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo kuwapatia ninyi upozi.4 Mose 28:15.
23Hao sharti mwatoe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya asubuhi inayotolewa kila siku.
24Hao na mwatoe kila siku siku hizo saba kuwa chakula cha moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana; nao na watolewe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na kinywaji chake cha tambiko.
25Siku ya saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Ng'ombe za tambiko za sikukuu ya Pentekote.26Siku ya malimbuko, mtakapomtolea Bwana vilaji vipya vya tambiko, ndio sikukuu yenu ya majuma saba; hapo na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.3 Mose 23:15-21.
27Tena na mtoe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza Bwana: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja.
28Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe na vibaba sita vya dume moja la kondoo,
29tena vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
30Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwapatia ninyi upozi.4 Mose 28:15.
31Hao na mwatoe pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na kilaji chake cha tambiko; nao sharti wawe pasipo kilema, tena mtoe navyo vinywaji vyao vya tambiko.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.