1Mungu, mpe mfalme kuamua, kama unavyoamua! Naye mwana wa mfalme mpe wongofu ulio kama wako!
2Awahukumu walio ukoo wako kwa wongofu, nayo mashauri yao wanyonge wako ayanyoshe!
3Milima iwe yenye matengemano ya kuwagawia watu, navyo vilima vilevile kwa nguvu ya wongofu!
4Walio wanyonge kwao atawaamulia, nao wana wao maskini atawaokoa, lakini wakorofi atawaponda.
12Kwani atamwopoa maskini amliliaye, hata mnyonge akosaye mwenye kumsaidia.
15Na akae akiwa mwenye uzima, wamgawie nazo dhahabu za Arabia! Na wamwombee pasipo kukoma, wamtukuze siku zote.
18Na atukuzwe Bwana Mungu, Mungu wa Isiraeli!
Yeye peke yake ndiye afanyaye vioja!
19Jina lake tukufu na litukuzwe kale na kale!
Nchi zote na zijae utukufu wake! Amin. Amin.
20Huu ndio mwisho wa maombo ya Dawidi, mwana wa Isai.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.