1Neno la Bwana likanijia kwamba:
2Nenda kutangaza masikioni mwao Wayerusalemu kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nayakukumbukia magawio ya ujana wako na upendo wa uchumba wako, uliponifuata nyikani katika nchi isiyowezekana kupandwa mbegu.
3Hapo Waisiraeli walikuwa wamejitakasa kuwa wa Bwana, wakawa malimbuko ya mavuno yake; wote waliotaka kuwala wakakora manza, mabaya yakawajia; ndivyo, asemavyo Bwana.
4Lisikilizeni Neno la Bwana ninyi wa mlango wa Yakobo nanyi vizazi vyote vya mlango wa Isiraeli!
5Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Baba zenu waliona mapotovu gani kwangu wakiniacha mbali wakaja kuyafuata yasiyo maana na kufanya wenyewe yasiyo maana?
29Mbona unanigombeza? Ninyi nyote mmenitengua; ndivyo, asemavyo Bwana.
30Imekuwa ya bure, nikiwapiga wana wenu, maana hawakuonyeka, panga zenu zikawala wafumbuaji wenu, kama simba wanavyoangamiza.Yes. 1:5.
31Ninyi mlio uzao mbaya, liangalieni Neno la Bwana! Je? Nimegeuka kuwawia Waisiraeli kama nyika au kama nchi yenye giza? Kwa sababu gani walio ukoo wangu husema: Tumekwisha kujiendea, haturudi kwako tena.
32Je? Yuko mwanamwali asahauye kujipamba au mchumba asahauye kuvaa yapasayo ndoa? Nao walio ukoo wangu wamenisahau siku zisizohesabika.
33Unajuaje kuitengeneza njia yako vizuri ukitafuta wapenzi? Kweli hivyo ndivyo, ulivyojifundisha mabaya nayo katika njia zako.
34Kumbe hata mapindo ya nguo zako yameshikwa na damu zao wakiwa waliouawa pasipo makosa yao yo yote. Nao hukuwapata, wakipokonya, ila ni mambo yayo hayo.
35Kisha ukasema: Sikukosa kamwe: Kwa hiyo makali yake yameondoka kwangu. Na unione, nikikupatiliza kwa kusema kwako: Sikukosa!Yes. 43:26.
36Mbona unatangatanga sana, uigeuze njia yako? Hata Wamisri watakutia soni, kama Waasuri walivyokutia soni.
37Huko nako utatoka, mikono yako ikiwa kichwani, kwani Bwana amewakataa, uliowakimbilia; kwa hiyo hakuna, utakachokipata kwao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.