Malaki 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Siku ya Bwana.

1*Kwani mtaiona hiyo siku, ikija na kuwaka moto kama wa tanuru; ndipo, waliomsahau Mungu nao wote waliofanya maovu watakapokuwa makapi, siku hiyo ijayo itakapoyateketeza, isisaze wala mizizi wala matawi yao hao; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.

2Lakini ninyi mliogopao Jina langu jua la wongofu litawachea, nalo litakuwa linao uponya mabawani mwake; ndipo, mtakapochezacheza kama ndama watokao zizini.

4Yakumbukeni Maonyo ya mtumishi wangu Mose, niliyomwagiza kule Horebu, awafundishe Waisiraeli wote maongozi na maagizo.

5Na mwone, nikimtuma mfumbuaji Elia kuja kwenu, siku kubwa ya Bwana iogopeshayo itakapokuwa haijatimia bado.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help