1Makali ya Bwana yakawawakia Waisiraeli tena, kwa hiyo akamhimiza Dawidi kuwaponza akimwambia: Wahesabu Waisiraeli na Wayuda!Dawidi anamtambikia Bwana penye kupuria ngano pa Arauna.
18Siku hiyo Gadi akaja kwake Dawidi, akamwambia: Mtengenezee Bwana pa kutambikia penye kupuria ngano pa Myebusi Arauna!
19Kwa hilo neno la Gadi Dawidi akapanda, kama Bwana alivyoagiza.
20Arauna alipochungulia akamwona mfalme na watumishi wake, wakipanda kuja kwake; ndipo, Arauna alipotoka, akamwangukia mfalme usoni pake hapo chini.
21Kisha Arauna akauliza: Ni kwa sababu gani, bwana wangu mfalme akija kwa mtumishi wake? Dawidi akamwambia: Ninataka kununua kwako hapa pako pa kupuria ngano, nijenge pa kumtambikia Bwana, huku kuuawa kwa watu kukomeshwe.
22Arauna akamwambia Dawidi: Bwana wangu mfalme na apachukue tu, atambike, kama yalivyo mema machoni pake. Tazama, nakupa hawa ng'ombe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, nayo haya magari na vyombo vya ng'ombe nakupa kuwa kuni.
23Haya yote, mfalme, Arauna anampa mfalme. Kisha Arauna akamwambia mfalme: Bwana Mungu wako na apendezwe na wewe!
24Lakini mfalme akamwambia Arauna: Sivyo, ila nitapanunua kabisa kwako na kulipa kilicho kiasi chake; sitamtolea Bwana Mungu wangu ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, nisizozilipa. Kisha Dawidi akapanunua hapo pa kupuria pamoja na ng'ombe kwa fedha 50.
25Kisha Dawidi akamjengea Bwana hapo mahali pa kumtambikia, akamtolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vya tambiko vya kumshukuru. Ndipo, Bwana aliposikia akiombwa kwa ajili ya nchi hiyo, nako kuuawa kwao Waisiraeli kukakomeshwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.