1Bwana, ukisimama mbali, ni kwa sababu gani? Ukaja kujificha siku za kusongeka?
7Kinywa chake hujaa viapizo na mapunjo ya kudanganya watu, nayo makorofi na maovu yamo chini ya ulimi wake.
12Inuka, Bwana! Nao mkono wako uunyoshe, Mungu! Usiwasahau hao walio wanyonge!
13Sababu gani wakubeze, Mungu, wao wasiokucha wakisema mioyoni mwao: Hutalipisha?
14Kwa kuyatazama makorofi na maumivu umeyaona hayo, namo mkononi mwako ndimo, yalimo sasa; akorofikaye hukuachilia wewe mambo yake yote, naye aliyefiwa na wazazi, wewe humwia msaidiaji.Sh. 68:6; 2 Mose 22:23.
15Ivunje mikono yake asiyekucha kwa kuwa mbaya! Yalipize mabezo yake, yasionekane tena!Sh. 37:10,36.
16Bwana ni mfalme siku zote zitakazokuwa kale na kale, wamizimu sharti waangamie nchini kwake.Sh. 99:1.
17Wanyonge umewasikia, Bwana, walipokupigia kite, ukaishikiza mioyo yao na kuwasikiliza kwa masikio yako.
18Huwaamulia waliofiwa na wazazi, nao wakorofikao, mtu asifulize tena kujivuna huku nchini.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.