3 Mose 19 - Swahili Roehl Bible 1937

Maelezo ya maagizo kumi.

1Bwana akamwambia Mose kwamba:

2Sema na mkutano wote wa wana wa Isiraeli, uwaambie: Sharti mwe watakatifu, kwani mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu.

13Usimkorofishe mwenzio na kumnyang'anya. Mshahara wa kazi, uliyofanyiziwa, usilale nao, mpaka kuche.

15Msifanye mapotovu mashaurini mkiupendelea uso wa mkiwa au mkimtukuza mkuu, ila umwamulie mwenzako kwa wongofu.

19Yaangalieni maongozi yangu! Usiwaache nyama wako wa kufuga, walale pamoja na nyama wengine, wala shamba lako usilipande mbegu za namna mbili, wala mwilini mwako usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za namna mbili.

20Mtu akilala kwa mwanamke kijakazi na kumpa mimba, naye alikuwa ameposwa na mtu mwingine, basi, akiwa hakukombolewa wala hakufunguliwa kujiendea, na wapatilizwe, lakini wasiuawe, kwa kuwa yule mwanamke hakufunguliwa kujiendea.

21Naye mume sharti apeleke dume la kondoo hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi ya kumtolea Bwana kwa ajili ya manza, alizozikora.

22Naye mtambikaji na ampatie upozi na kumtoa yule dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi mbele ya Bwana kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa; ndipo, atakapoondolewa hilo kosa lake, alilolikosa.

23Mtakapoingia katika nchi ile mtapanda miti yo yote yenye matunda ya kula, lakini kwanza iacheni yenye magovi yao, ndio matunda yao, miaka mitatu mwiwazie kuwa haijatahiriwa, isiliwe.

24Katika mwaka wa nne matunda yao yote pia yawe matakatifu ya kumtolea Bwana shukrani.

25Katika mwaka wa tano mtaweza kuyala matunda yao; ndivyo, mtakavyojiongezea mapato yao. Mimi Bwana ni Mungu wenu.

26Msile cho chote kilicho chenye damu bado. Msipige bao, wala msiagulie mawingu.

32Mbele yake mwenye mvi sharti uinuke, naye aliye mzee sharti umheshimu usoni pake kwa kumwogopa Mungu wako. Mimi ni Bwana.

33Mgeni akikaa ugenini kwenu katika nchi yenu, msimwonee,

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help