1Kulikuwa na mwanamke wa wanafunzi wa wafumbuaji, akamlilia Elisa kwamba: Mume wangu, mtumishi wako, amekufa, nawe unajua, ya kuwa mtumishi wako alikuwa mwenye kumcha Bwana; tena mtu, aliyemkopa, amekuja kuwachukua wanangu mawili, wawe watumwa wake.
2Elisa akamwuliza: Nikufanyizie nini? Niambie, nyumbani mwako unavyo vyombo gani? Akajibu: Kijakazi wako hanacho cho chote nyumbani, ni kitungi cha mafuta tu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.