1Akaondoka huko, akaja mipakani kwa Yudea na ng'ambo ya Yordani. Walipomkusanyikia tena makundi ya watu, akawafundisha tena, kama alivyozoea.
7Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake,
Mwenye mali nyingi.(17-31: Mat. 19:16-30; Luk. 18:18-30.)
17*Alipotoka na kufika njiani, mmoja akamjia mbio, akampigia magoti, akamwuliza: Mfunzi mwema, nifanye nini, niurithi uzima wa kale na kale?
18Yesu akamwambia: Unaniitaje mwema? Hakuna aliye mwema, asipokuwa Mungu peke yake tu.
19Maagizo unayajua, ya kwamba: Usiue! Usizini! Usiibe! Usisingizie! Usipunje! Mheshimu baba yako na mama yako!Malipo.
28Petero akaanza kumwambia: Tazama, sisi tumeviacha vyote, tukakufuata wewe.
29Ndipo, Yesu aliposema: Kweli nawaambiani: Hakuna mtu aliyeacha nyumba au kaka au dada au mama au baba au wana au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Utume mwema,
30asiporudishiwa na kuongezwa mara mia siku hizi za kuwapo huku nchini nyumba na kaka na dada na mama na wana na mashamba, hata akiwa anafukuzwafukuzwa. Tena siku zile zitakazokuja ataupata nao uzima wa kale na kale.
31Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, nao walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
Mwana wa mtu atateswa.(32-34: Mat. 20:17-19; Luk. 18:31-34.)32Walipokuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa anatangulia mbele yao. Nao wakashikwa na kituko, wakamfuata na kuogopa. Akawachukua tena wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia mambo yatakayompata,Mar. 9:31; Yoh. 11:16,55.
33akasema: Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu. Huko Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwao watambikaji wakuu na waandishi, nao watamhukumu, auawe; kwa hiyo watamtia mikononi mwa wamizimu.
34Ndio watakaomfyoza na kumtemea mate na kumpiga viboko na kumwua. Naye, siku tatu zitakapopita, atafufuka.
35 Yakobo na Yohana.(35-45: Mat. 20:20-28.)35*Yakobo na Yohana, wana wa Zebedeo, wakamsogelea wakimwambia: Mfunzi, twataka, ufufanyie lo lote, tutakalokuomba.
36Alipowauliza: Mwataka, niwafanyie nini?
37wakamwambia: Utuketishe mmoja kuumeni na mmoja kushotoni kwako katika utukufu wako!
38Yesu akawaambia: Hamjui, mnaloliomba. Mwaweza kukinywa kinyweo, ninachokinywa mimi, au kubatizwa ubatizo, ninaobatizwa mimi?Mar. 14:36; Luk. 12:50; Rom. 6:3.
39Walipomwambia: Twaweza, Yesu akawaambia: Kinyweo, ninachokinywa mimi, mtakinywa nao ubatizo, ninaobatizwa mimi, mtabatizwa;Tume. 12:2; Ufu. 1:9.
40lakini kumketisha mtu kuumeni au kushotoni kwangu hii si kazi yangu, ila hupewa walioandaliwa.
41Wenzao kumi walipoyasikia wakaanza kumkasirikia Yakobo na Yohana.
42Yesu akawaita, wamjongelee, akawaambia: Mnajua: wanaotazamwa kuwa wafalme wa mataifa huwatawala, nao wakubwa wao huwatumikisha kwa nguvu. Kwenu ninyi visiwe hivyo!Luk. 22:25-27.
43Ila mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu sharti awe mtumishi wenu!Mar. 9:35.
44Naye anayetaka kuwa wa kwanza kwenu sharti awe mtumwa wao wote!
45Kwani naye Mwana wa mtu hakuja, atumikiwe, ila amekuja kutumika na kuitoa roho yake kuwa makombozi ya watu wengi.
Kipofu wa Yeriko.(46-52: Mat. 20:29-34; Luk. 18:35-43.)46Wakafika Yeriko. Nao walipotoka Yeriko, yeye na wanafunzi wake na kundi la watu wengi, Bartimeo, mwana wa Timeo, aliyekuwa kipofu alikaa njiani kando akiomba sadaka.
47Aliposikia, ya kuwa Yesu wa Nasareti yuko, akaanza kupaza sauti na kusema: Yesu, mwana wa Dawidi, nihurumie!
48Wengi walipomkaripia, anyamaze, yeye akakaza sana kupaza sauti: Mwana wa Dawidi, nihurumie!
49Ndipo, Yesu aliposimama, akasema: Mwiteni! Wakamwita kipofu, wakamwambia: Tulia moyo, inuka! anakuita.
50Naye akaitupa kanzu yake, akainuka upesi, akaja kwa Yesu.
51Yesu alipomwuliza akisema: Wataka, nikufanyie nini? kipofu akamwambia: Mfunzi mkuu, nataka, nipate kuona.
52Yesu akamwambia: Enenda! Kunitegemea kwako kumekuponya. Mara akapata kuona, akamfuata njiani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.