1Alipoinua macho akaona, wenye mali walivyotia sadaka zao katika sanduku ya vipaji.
2Akaona hata mwanamke mjane aliyekuwa mkiwa, alivyotia mle visenti viwili.
3Ndipo, aliposema: Kweli nawaambiani: Huyu mjane mkiwa ametia mengi kuliko wote.
4Kwani hao wote walitoa mali katika mali zao nyingi, wakazitia penye sadaka, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vilivyomlisha.
Mambo yatakayokuja.(5-24: Mat. 24:1-21; Mar. 13:1-19.)5Wengine waliposema, Patakatifu palivyokuwa pamepambwa na mawe mazuri na mapambo mengine, ndipo, aliposema:
6Je? Mwayatazama haya? Siku zitakuja, ambapo halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.
7Wakamwuliza wakisema: Mfunzi, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo ni nini, hayo yatakapotimia?
8Naye akasema: Angalieni, msipotezwe! Kwani wengi watakuja kwa Jina langu na kusema: Mimi ndiye, nazo siku zimekwisha kufika. Msiwafuate hao!
9Nanyi mtakaposikia vita na mainukiano, msitukutike! Kwani hayo sharti yawepo kwanza; lakini mwisho hauji upesi.
10Ndipo alipowaambia: Watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme.
11Mahali penginepengine patakuwa na matetemeko makuu, pengine na kipindupindu, pengine na njaa. Hata vielekezo vikubwa vitatokea mbinguni vya kuogofya.
12Lakini hayo yote yatakapokuwa hayajatimia bado, watawanyoshea mikono, wawakamate na kuwakimbiza, wawapeleke nyumbani mwa kuombea namo mabomani, wawaweke mbele yao wafalme na mabwana wakubwa kwa ajili ya Jina langu.(25-28: Mat. 24:29-30; Mar. 13:24-26.)
25*Kutakuwa na vielekezo vya jua na vya mwezi na vya nyota. Huku nchini watu wa mataifa yote watapotelewa na mioyo wasipojua maana, mawimbi ya bahari yatakapokaza kuvuma na kutukutika.
26Ndipo, watu watakapozimia kwa woga na kwa kuyangoja mambo yatakayopajia pote, wanapokaa, kwani hata nguvu za mbingu zitatukutishwa.
27Hapo ndipo, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja katika wingi mwenye nguvu na utukufu mwingi.(29-33: Mat. 24:32-35; Mar. 13:28-31.)
29Kisha akawaambia mfano: Utazameni mkuyu na miti yote!
30Mnapoiona, ikichipua, mnatambua wenyewe, ya kuwa siku za vuli zimekwisha kuwa karibu.
31Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo, yakiwapo, tambueni, ya kuwa ufalme wa Mungu umewafikia karibu!
32Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma, mpaka yatakapokuwapo yote.
33Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.
37Akawa kila siku akifundisha Patakatifu, lakini usiku hutoka na kulala kwenye mlima unaoitwa Wa Michekele.
38Nao watu wote walikuwa wakimwendea asubuhi pale Patakatifu, wamsikilize.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.