1 Mose 37 - Swahili Roehl Bible 1937

Ndoto za Yosefu.

1Yakobo akakaa katika nchi hiyo, baba yake alikokaa ugenini, ndio nchi ya Kanaani.

2Hivi ni vizazi vya Yakobo: Yosefu alipopata miaka 17, akachunga mbuzi na kondoo pamoja na kaka zake; huyu kijana Yosefu alipokuwa pamoja na wana wa Biliha nao wana wa Zilpa, wakeze baba yake, yeye Yosefu akamsimulia baba yao mambo yao mabaya.

3Naye Isiraeli alimpenda Yosefu kuliko wanawe wote, kwa kuwa ni mwanawe wa uzee wake; kwa hiyo akamshonea kanzu ya nguo za rangi.

4Kaka zake walipoona, ya kuwa baba yao alimpenda kuliko ndugu zake, wakamchukia, hawakuweza kusema naye kwa upole.

5Kisha Yosefu akaota ndoto, akawasimulia kaka zake; ndipo, walipozidi kumchukia,

6kwani aliwaambia: Isikieni ndoto hii, niliyoiota!

7Nimeona, sisi tulikuwa shambani tukifunga miganda; mara mganda wangu ukainuka, ukasimama, nayo miganda yenu ikauzunguka, ikazungukia mganda wangu.

8Ndipo, kaka zake walipomwambia: Je? Unataka kuwa mfalme wetu, ututawwale? Wakazidi kumchukua sana kwa ajili ya ndoto zake na kwa ajili ya maneno yake.

9Akaota tena ndoto nyingine, akaisimulia nayo kaka zake akiwaambia: Tazameni! Nimeota ndoto nyingine, nikaona, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikiniangukia.

10Alipomsimulia baba yake nao kaka zake ndoto hizi, baba yake akamkemea, akamwambia: Hiyo ndoto yako, uliyoiota, ni ndoto gani? Je? mimi na mama yako na kaka zako tuje, tukuangukie chini?

11Ndipo, kaka zake walipomwonea wivu, lakini baba yake akayashika maneno hayo na kuyaangalia.

Kuuzwa kwake Yosefu.

12Kisha kaka zake walipokwenda kuwachnga mbuzi na kondoo wa baba yao huko Sikemu,

29Rubeni aliporudi hapo shimoni, akaona, ya kama Yosefu hayumo; ndipo, alipozirarua nguo zake,1 Mose 44:13; 2 Sam. 1:11.

30akarudi kwa ndugu zake, akawaambia: Mtoto hayumo, mimi nami niende wapi?

Kusikitika kwake Yakobo.

31Kisha wakaichukua kanzu ya Yosefu, wakachinja dume la mbuzi, wakaichovya hiyo kanzu katika damu yake.

32Kisha wakaituma hiyo kanzu ya nguo za rangi kumpelekea baba yao, wakamwambia: Nguo hii tumeiokota; itazame, kama ndiyo kanzu ya mwanao, au kama siyo!

33Akaitambua, akasema: Ni kanzu ya mwanangu! Nyama mkali amemla, Yosefu ameraruliwa kweli!1 Mose 37:20.

34Ndipo, Yakobo alipozirarua nguo zake, akavaa gunia kiunoni, akamwombolezea mwanawe siku nyingi.1 Mose 37:29.

35Wakainuka wanawe wote wa kiume nao wote wa kike, wamtulize moyo, lakini akakataa kutulizwa moyo akisema: Nitashuka mwenye ukiwa huko kuzimuni, mwanangu aliko. Ndivyo, baba yake alivyomlilia.

36Wale Wamidiani wakamwuza huko Misri kwa Potifari aliyekuwa mtumishi wa nyumbani mwa Farao na mkuu wao waliomlinda Farao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help