1Kulikuwa na mtu jina lake Anania, na mkewe Safira; huyu alipouza kiunga
2akaficha fungu la fedha, alizozipata, naye mkewe alivijua. Kisha akaleta fungu moja, akaliweka miguuni pa mitume.
34*Kisha pakainuka hapo penye wakuu Fariseo, jina lake Gamalieli; ni mfunzi wa Maonyo mwenye cheo kwa watu wote, akaagiza, wale watu wapelekwe nje kidogo.Tume. 22:3.
35Kisha akawaambia: Waume Waisiraeli, jilindeni kwa ajili ya hayo, mtakayowatendea watu hawa!
36Kwani mbele ya siku hizi aliondokea Teuda, akajiwazia, kwamba yeye ndiye mtu, nao watu waliomfuata wakapata kama 400. Alipouawa, wote waliomtii wakatawanyika, wakapoteapotea, tena hakuna kitu.
37Kisha katika siku za kuandikiwa kodi aliondokea Yuda Mgalilea, akatenga kikundi cha watu, wamfuate yeye. Naye alipoangamia, wote waliomtii wakatawanyika nao.
38Kwa hiyo sasa nawaambiani: Mtengamane na watu hawa, mwaache! Kwani mawazo hayo au kazi hizo zikiwa zimetoka kwa watu zitakoma;Mat. 15:13.
39lakini zikiwa zimetoka kwake Mungu, hamwezi kuwakomesha, msije mkaonekana, ya kuwa mnagombana na Mungu.Tume. 9:5.
40Ndipo, walipomwitikia, wakawaita wale mitume, wakawapiga, wakawakemea, wasiseme tena mambo ya Jina la Yesu, kisha wakawafungua.Tume. 22:19.
41Wao wakatoka machoni pa wakuu wakichangamka, kwa sababu Mungu amewapa kutwezwa kwa ajili ya Jina lake.Mat. 5:10-12; 1 Petr. 4:13.
42Siku zote hawakuacha kufundisha na kuutangaza Utume mwema wa Yesu Kristo hapo Patakatifu na nyumbani mo mote.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.