1Siku sita mbele ya kuwa Pasaka Yesu akaenda Betania, ndiko kwao Lazaro, Yesu aliyemfufua katika wafu.Njama ya kumwua Lazaro.
9Kundi la Wayuda wengi walipotambua, ya kuwa yuko kule, wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila walitaka kumwona naye Lazaro, aliyemfufua katika wafu.
10Kwa hiyo watambikaji wakuu wakala njama ya kumwua hata Lazaro.
11Kwani kwa ajili yake yeye Wayuda wengi wakaenda kule, wakamtegemea Yesu.
Kuingia Yerusalemu.(12-19: Mat. 21:1-11; Mar. 11:1-10; Luk. 19:29-40.)12*Kesho yake wale watu wengi walioijia sikukuu waliposikia, ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,
13wakachukua makuti ya mitende, wakatoka kumwendea, wakapaza sauti:
Hosiana! Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!
Ndiye mfalme wa Isiraeli!Wagriki wanamwendea Yesu.
20*Miongoni mwao waliopanda kutambika siku za ile sikukuu mlikuwa na Wagriki.
21Hao wakamjia Filipo wa Beti-Saida wa Galilea, wakambembeleza wakisema: Bwana, twataka kumwona Yesu.Wapenzi na wachukivu wa Yesu.
37Yesu alipokwisha kuyasema haya, akaenda zake, akajificha, wasimwone tena. Lakini ijapokuwa amefanya mbele yao vielekezo vingi kama hivyo, hawakumtegemea.
38Imekuwa hivyo, neno, mfumbuaji Yesaya alilolisema, lipate kutimia:
Bwana, yuko nani anayeutegemea utume wetu?
Tena yuko nani aliyefumbuliwa, mkono wa Bwana
unayoyafanya?
40Amewapofua macho, akaishupaza mioyo yao,
wasije wakaona kwa macho yao, au wakajua maana kwa mioyo
yao, au wakageuka, nami nikawaponya.
41Yesaya aliyasema hayo, kwani aliuona utukufu wake, akayasema mambo yake yeye.Mungu amemtuma Yesu.
44Lakini Yesu alipaza sauti, akasema: Anayenitegemea hanitegemei mimi, ila humtegemea yule aliyenituma.
45Tena, anayeniona mimi humwona yule aliyenituma.Yoh. 14:9.
46Mimi nimekuja ulimwenguni kuwa mwanga, kila anitegemeaye asikae gizani.Yoh. 12:35.
47Mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu. Kwani sikujia kuuhukumu ulimwengu, ila nimejia kuuokoa ulimwengu.Yoh. 3:17; Luk. 9:56.
48Anikataaye, asiyapokee maneno yangu, anaye atakayemhukumu. Neno, nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
49Kwani mimi sikuyasema maneno yangu, ila Baba mwenyewe aliyenituma ameniagiza, nitakayoyasema na kuyafundisha.
50Nami nayajua, aliyoyaagiza, ya kuwa ni uzima wa kale na kale. Basi, ninayoyasema, ninayasema, kama Baba alivyoniambia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.