3 Yohana 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Anwani.

1Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo, mpendwa wangu, ninayempenda kweli.Kuwakaribisha wageni kunafaa.

2Mpendwa, kuliko yote nakuombea, ukae vema na kuwa mzima, kama roho yako inavyokaa vema.

3Kwani nalifurahi sana, ndugu walipokuja na kutushuhudia, kuwa u mwenye kweli, kama wewe unavyoishika njia ya kweli.Diotirefe na Demetirio.

9Yako mengine, niliyoyaandikia wateule. Lakini Diotirefe anayependa kuwa mkubwa wao hatusikii sisi.

10Kwa hiyo nitakapokuja nitazikumbusha kazi zake, anazozifanya akituteta sisi kwa maneno mabaya. Nayo hayo hayamtoshi: mwenyewe hawapokei ndugu, nao wanaotaka kuwapokea huwazuia, kisha huwafukuza kwenye wateule.

11Mpendwa, usiuige uovu, ila uuige wema! Anayefanya yaliyo mema ni wa Kimungu; anayefanya yaliyo maovu hakumwona Mungu.

13Nalikuwa nayo mengi ya kukuandikia, lakini sitaki kukuandikia tu kwa wino na kalamu,2 Yoh. 12.

14ila nangojea, nikuone upesi, tusemeane kinywa kwa kinywa.

15Utengemano ukukalie! Wapenzi wanakusalimu. Nisalimie wapenzi kila kwa jina lake!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help