1Wafilisti walipopigana na Waisiraeli, watu wa Waisiraeli wakawakimbia Wafilisti kwa madonda waliyopigwa, wakaanguka wakafa kule mlimani kwa Gilboa.
2Wafilisti wakawafuata na kuandamana na Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua wana wa Sauli: Yonatani na Abinadabu na Malkisua.
3Mapigano yakawa makali hapo, Sauli alipokuwa; wapiga mishale walipomwona, akaumizwa sana nao wapiga mishale.
4Ndipo, Sauli alipomwambia mchukua mata yake: Uchomoe upanga wako, unichome nao, hao wasiotahiriwa wasije kunichoma na kunichezea vibaya! Mchukua mata yake alipokataa kwa kuogopa sana, Sauli akausimika upanga, akauangukia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.