2 Mambo 6 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba kwake Salomo(1 Fal. 8:12-53.)

1Ndipo, Salomo aliposema: Bwana alisema, ya kuwa hukaa mawinguni mwenye weusi.

2Nami nimekujengea Nyumba ya kukaa, iwe Kao lako la kukaa humu kale na kale.

3Kisha mfalme akaugeuza uso wake, akaubariki mkutano wote wa Waisiraeli, nao wote wa mkutano wa Waisiraeli walikuwa wamesimama.

4Akasema: Atukuzwe Bwana Mungu wa Isiraeli! Aliyomwambia baba yangu Dawidi kwa kinywa chake, ameyatimiza kwa mikono yake, ya kwamba:

5Tangu siku ile, nilipowatoa walio ukoo wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji katika mashina yote ya Isiraeli, ndimo wanijengee Nyumba, Jina langu likae humo, wala sikuchagua mtu wa kuwatawala walio ukoo wangu wa Waisiraeli.

6Kisha nikachagua Yerusalemu, Jina langu liwemo, nikamchagua Dawidi wa kuwatawala walio ukoo wangu wa Waisiraeli.

7Baba yangu Dawidi akawaza moyoni kulijengea Jina la Bwana Mungu wa Isiraeli nyumba,

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help