1 Samweli 25 - Swahili Roehl Bible 1937

Samweli anakufa.

1Siku zile Samweli akafa; ndipo, Waisiraeli wote walipokusanyika kumwombolezea na kumzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Dawidi akaondoka, akatelemka kwenda nyikani kwa Parani.Ujinga wa Nabali.

2Kule Maoni kulikuwa na mtu, nako, alikopatia mali, ni Karmeli; mtu huyo alikuwa mkuu kabisa mwenye kondoo 3000 na mbuzi 1000. Naye siku hizo alikuwa huko Karmeli akiwakata kondoo wake manyoya.

3Huyo mtu jina lake Nabali, naye mkewe jina lake Abigaili; huyu mkewe alikuwa mwenye akili njema na mwenye umbo zuri, lakini yule mume alikuwa mkorofi mwenye matendo mabaya tu, naye ni wa mlango wa Kalebu.

4Dawidi aliposikia kule nyikani, ya kuwa Nabali yumo katika kukata manyoya ya kondoo wake,

5Dawidi akatuma vijana kumi; Dawidi akawaambia hao vijana: Pandeni Karmeli, mwende kwa Nabali kunisalimia kwake!

6Mmwambieni huyu ndugu yangu: Hujambo wewe? Nao wa mlango wako hawajambo? Nao wote walio wako hawajambo?

7Sasa nimesikia, ya kuwa wanakukatia manyoya ya kondoo wako; basi, hao wachungaji wako walikuwa kwetu sisi, nasi hatukuwafanyizia kibaya cho chote, wala hakikupotea cho chote kwao siku zote, walipokuwa huku Karmeli.

8Waulize vijana wako, nao watakuambia, kwa hiyo hawa vijana na waone upendeleo machoni pako! Kwani tumekuja siku iliyo njema; mkono wako utakayoyaona, tupe sisi watumishi wako naye mtumishi wako Dawidi!

9Vijana wa Dawidi walipofika kwake wakamwambia Nabali hayo maneno yote katika jina la Dawidi, kisha wakanyamaza.

10Lakini Nabali akawajibu vijana wa Dawidi kwamba: Dawidi ni nani? Mwana wa Isai ni nani? Leo watumwa waliotoroka kwa bwana zao ni wengi.

11Sasa je? Vilaji vyangu na vinyaji vyangu na vinono vyangu, nilivyowachinjia wanaokata manyoya ya kondoo wangu, nivichukue, niwape watu, nisiowajua, wanakotoka?

12Ndipo, vijana wa Dawidi walipogeuka kurudi kwao; walipofika wakampasha habari hizo zote.

13Ndipo, Dawidi alipowaambia watu wake: Jifungeni kila mtu upanga wake! Nao wakajifunga kila mtu upanga wake, hata Dawidi akajifunga upanga wake; wakamfuata Dawidi watu kama 400 kwenda naye, wengine 200 wakasalia kwenye mizigo yao.

Abigaili anampoza Dawidi kwa werevu wake.

14Kijana mmoja miongoni mwao wale vijana akamsimulia Abigaili, mkewe Nabali, kwamba: Tazama! Dawidi ametuma wajumbe toka nyikani, waje kumsalimia bwana wetu, lakini akawafokea.

15Nao wale watu wametufanyizia mema sana, hawakutufanyizia kibaya cho chote, wala hakikupotea kwetu cho chote siku zote, tulizotembea nao tulipokuwa porini.

16Walikuwa kwetu kama boma usiku na mchana siku zote, tulizokuwa kwao tukichunga kondoo.

17Sasa yajue hayo, uone utakayoyafanya! Kwani yako mabaya yaliyokwisha kutengenezwa ya kumpata bwana wetu na mlango wake wote; lakini yeye ni mtu asiyefaa, hatuwezi kusema naye.

18Ndipo, Abigaili alipojihimiza, akachukua mikate 200 na mitungi 2 ya mvinyo na kondoo 5 waliokwisha kutengenezwa na pishi 5 za bisi na maandazi 100 ya zabibu na 200 ya kuyu, yote pia akapagaza punda.

19Kisha akawaambia vijana wake: Nitangulieni! Mimi nitawafuata nyuma. Lakini mumewe Nabali hakumwambia neno.

20Ikawa, alipokuwa amepanda punda wake na kutelemka mahali palipofichwa na mlima, naye Dawidi na watu wake walikuwa wakitelemka papo hapo upande wa huko; ndivyo, alivyokutana nao.

21Dawidi akawa akiwaza moyoni kwamba: Kumbe mali zote za mtu huyu nimezilinda nyikani bure tu, yote pia yaliyokuwa yake hayakupotea hata moja, naye hayo mema akayalipa kwa kunifanyizia mabaya.

22Mungu na awafanyizie wachukivu wote wa Dawidi hivi na hivi, nikisaza mpaka mapambazuko ya kesho mtu mmoja tu wa kiume kwao wote walio watu wake!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help