Mashangilio 83 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba msaada vitani.Wimbo wa Asafu wa kushukuru.

1Mungu usijinyamazie tu! Wala usiache kujibu! Usitulie tu, wewe Mungu!

2Kwani tazama, adui zako wanafanya fujo! Wachukivu wako wanainua vichwa!

3Wanakula njama ya kuwaangamiza walio ukoo wako, wanawapigia mashauri mabaya wao, uliowaficha.

13Mungu wangu, wafanye kuwa mavumbi yachukuliwayo na kimbunga au kuwa makapi, yakipeperushwa na upepo,

14wawe kama moto unaochoma mwitu, au kama ndimi za moto ziwashazo milima!

15Vivyo hivyo uwakimbize kwa nguvu zako zilizo za kimbunga! Uwastushe, wazimie kwa nguvu zako zilizo za chamchela!

16Nyuso zao sharti ziwaive kwa kutwezwa, mpaka walitafute Jina lako, wewe Bwana.

17Sharti wapatwe na soni pamoja na mastuko kale na kale! Sharti waumbuliwe, mpaka waangamie!

18Ndivyo, watu watakavyolitambua Jina lako kuwa Bwana, kwa kuwa wewe peke yako u mkuu katika nchi zote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help