Yeremia 25 - Swahili Roehl Bible 1937

Wayuda watatumikishwa Babeli miaka 70.

1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kwa ajili ya ukoo wote wa Yuda katika mwaka wa nne wa Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, nao ulikuwa mwaka wa kwanza wa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli.

2Naye mfumbuaji Yeremia akaliambia wao wote wa ukoo wa Yuda nao wote wakaao Yerusalemu kwamba:

3Kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa Yosia, mwana wa Amosi, mfalme wa Yuda, mpaka siku hii ya leo, hii miaka ishirini na mitatu yote neno la Bwana limenijia, nikawaambia pasipo kuchoka kila kulipokucha, lakini hamkusikia.

4Naye Bwana alituma kwenu watumishi wake wote waliokuwa wafumbuaji, naye aliwatuma pasipo kuchoka kila kulipokucha, lakini hamkusikia, wala hamkuyatega masikio yenu, mpate kusikia.

5Nao wakasema: Rudini kila mtu katika njia yake mbaya na kuyaacha matendo yenu mabaya! Ndipo, mtakapokaa katika nchi, Bwana aliyowapa ninyi na baba zenu, iwe yenu ya kale na kale kabisa.Kuangamia kwa Babeli.

12Ndivyo, asemavyo Bwana: Itakuwa, miaka 70 itakapopita, nitampatilizia mfalme wa Babeli na lile kabila lote mabaya yao, waliyoyafanya; hata nchi yao Wakasidi nitaigeuza kuwa peke yake tu kale na kale.

13Nitailetea nchi ile maneno yangu yote, niliyoyasema ya kuifanyizia, yaliyoandikwa humu kitabuni, mfumbuaji Yeremia aliyoyafumbua kwamba: Yatawajia hawa wamizimu wote.

14Kwani mataifa yenye watu wengi na wafalme wakuu watawatumikisha hawa nao, nami nitawalipisha kazi zao na matendo ya mikono yao.

Makali yatakayoyatokea makabila ya watu.

15Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli alivyoniambia: Kitwae mkononi mwangu kinyweo hiki cha mvinyo yenye ukali wa moto, ukinyweshe makabila yote ya watu, ambao nitakutuma kwenda kwao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help