Mifano 2 - Swahili Roehl Bible 1937
Mbaraka ya kutafuta ujuzi.
1*Mwanangu, ukiyapokea maneno yangu
na kuyashika maagizo yangu moyoni mwako,
2ukiutegea werevu wa kweli sikio lako,
ukauelekezea utambuzi moyo wako,
3ukiziita akili na kuipaza sauti yako, upate utambuzi,