1Hayo yalipomalizika, wakuu wakanitokea kwamba: Walio ukoo wa Isiraeli nao watambikaji na Walawi hawakujitenga kabisa na makabila ya nchi hizi walio na mambo mengi ya kutapisha mtu, wao Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori.
2Kwani wamejichukulia wenyewe na wana wao wanawake wa huko; ndivyo, walivyochanganya mazao matakatifu nayo yao ya makabila ya nchi hizi, nao wakuu wa watawalaji ndio walioanza kuinyosha mikono kuyavunja maagano ya Mungu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.