Mashangilio 53 - Swahili Roehl Bible 1937

Upumbavu wao wasiomcha Mungu.(Taz. Sh. 14.)Kwa mwimbishaji. Fundisho la Dawidi litakalo kuimbwa kama ombolezo.

1Mpumbavu husema moyoni mwake: Hakuna Mungu.

2Hawafai kitu, mapotovu yao hutapisha, anayefanya mema hayuko huko.

3Mungu huchungulia toka mbinguni, awatazame wana wa watu, aone, kama yuko mwenye akili anayemtafuta Mungu.

5Je? Wale wote wafanyao maovu hawataki kujitambua, wao wanaowala walio ukoo wangu, kama walavyo mkate? Lakini Mungu hawamtambikii!

6Patafika, watakapotetemeka kwa kustuka mastuko yasiyokuwa bado, kwa kuwa Mungu ataitapanya mifupa yao waliokuvizia, kwa kuwa Mungu atakuwa amewatupa, atawatia soni.

7Laiti wokovu wake Isiraeli utokee Sioni, Mungu awarudishe mateka walio wa ukoo wake! Ndipo, Yakobo atakaposhangilia, ndipo, Isiraeli atakapofurahi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help