Yohana 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Mgonjwa ziwani pa Betesida.

1*Kisha ilipokuwa sikukuu ya Wayuda, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.

2Kule Yerusalemu karibu ya Lango la Kondoo kulikuwako kiziwa kiitwacho Kiebureo Betesida; hapo palikuwa na vibanda vitano.

3Humo mlikuwa na wagonjwa wengi, kama vipofu na viwete na wenye kupooza; wote walilala mle wakingoja, maji yatukuswe.

4Kwani mara kwa mara palishuka malaika kiziwani, akayatikisa maji; hapo, maji yalipoisha kutikiswa, aliyeingia wa kwanza akapona ugonjwa wo wote uliomshika.

5Pale palikuwa na mtu aliyekuwa hawezi miaka 38.

6Yesu alipomwona huyo, anavyolala, akatambua, ya kuwa imemwishia hapo miaka mingi, akamwambia: Unataka kuwa mzima?

7Mgonjwa akamjibu: Bwana, sina mtu wa kunitia kiziwani, maji yanapotikiswa. Kila mara mimi ninapokwenda, mwingine hushuka mbele yangu.

8Yesu akamwambia: Inuka, jitwishe kitanda chako, upate kwenda zako!

10Lakini siku ile ilikuwa ya mapumziko. Kwa hiyo Wayuda walimwambia yule aliyeponywa: Leo ni siku ya mapumziko, huna ruhusa ya kukichukua kitanda.

19*Yesu akajibu, akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Hakuna, Mwana awezacho kukifanya kwa nguvu yake, asipokuwa amemwona Baba, anavyokifanya. Kwani yule anavyovifanya, hivyo naye Mwana huvifanya vile vile.

31Mimi ninapojishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu sio wa kweli.

32Yuko mwingine anayenishuhudia, nami naujua ushuhuda wake, alionishuhudia, ya kuwa ndio wa kweli.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help