1Mungu, lisikie lalamiko langu!
2Yaitikie nikuombayo!
3Kwenye mapeo ya nchi ninakuita, moyo wangu ukizimia. Unikweze mwambani! Kwani ni mrefu wa kunishinda.
4Kwani kimbilio langu ndiwe wewe, u mnara wenye nguvu machoni pao adui.Sh. 18:2-3; 71:3.
5Ninataka kuwamo katika kituo chako kale na kale, na kulikimbilia ficho lililomo mabawani mwako.Sh. 63:3.
6Kwani wewe, Mungu, umeyasikia niliyokuapia, ukanigawia fungu lao waliogopao Jina lako.
7Unamwongezea mfalme siku kwa siku, miaka yake iwe ya vizazi na vizazi.Sh. 21:5.
8Akiendelea machoni pake Mungu atakaa kale na kale. Agiza vya upole na vya kweli, vimsimamie!2 Sam. 7:16.
9Hivyo nitaliimbia Jina lako kale na kale na kuyalipa siku kwa siku niliyokuapia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.