Wagalatia 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Anwani.

1Mimi Paulo ni mtume, lakini sikutumwa na watu wala kwa agizo la mtu, ila nimetumwa kwa agizo lake Yesu Kristo nalo lake Mungu Baba aliyemfufua katika wafu.Kuitwa kwa Paulo.

11Ndugu zangu, nawatambulisha, ya kuwa Utume mwema uliotangazwa nami sio wa kimtu.

12Kwani nami sikuupokea kwa mtu, wala sikufundishwa, ila nimefunuliwa na Yesu Kristo.Tume. 9:1-15.

13Kwani mmesikia, nilivyoendelea hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, ya kuwa nalijipingia kuwafukuza wateule wa Mungu na kuwajengua.Tume. 26:4-20.

14Nami hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, nikapita wenzangu wengi, ambao tulizaliwa nao mwaka mmoja, maana nilikaza kujihimiza, niandamane nayo, tuliyoyapokea kwa baba zetu.

15Lakini Mungu alikuwa amenitenga hapo, nilipokuwa tumboni mwa mama yangu, akaniita, nigawiwe kipaji chake.Yer. 1:5; Rom. 1:1.

16Hapo, alipopendezwa kumfunua Mwana wake moyoni mwangu, kusudi nije, niwapigie wamizimu hiyo mbiu yake njema, papo hapo nikakata mawazo pasipo kuuliza mwili wangu ulio wenye nyama na damu,Gal. 2:7; Mat. 16:17.

17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwao waliokuwa mitume mbele yangu, ila nalikwenda Arabuni, kisha nikarudi tena Damasko.

18Miaka mitatu ilipokwisha kupita, nikapanda kwenda Yerusalemu, nijuane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano.Tume. 9:26.

19Lakini hakuna mtume mwingine, niliyemwona, asipokuwa Yakobo, nduguye Bwana.

20Lakini haya, ninayowaandikia, tazameni, Mungu anayajua, ya kuwa sisemi uwongo.

21Kisha nikafika upande wa Ushami na Kilikia.Tume. 9:30.

22Nami nilikuwa sijajulikana uso kwa uso nao wateule wake Kristo walioko Yudea.

23Ila walikuwa wamesikia tu: Yule aliyetufukuza kwanza sasa huipiga hiyo mbiu njema ya kumtegemea Bwana, alikokuwa amekujengua. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help