1Katika mwezi wa nane katika mwaka wa pili wa Dario neno la Bwana lilimjia mfumbuaji Zakaria, mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kwamba:
2Bwana alikuwa amewakasirikia sana baba zenu.
3Kwa hiyo uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Rudini kwangu! ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi; ndipo, nami nitakaporudi kwenu; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.Ono la pembe nne na la wafua vyuma wanne.
18Nilipoyainua macho yangu, nichungulie, mara nikaona pembe nne.
19Nikamwuliza malaika aliyesema na mimi: Za nini hizi? Akaniambia: Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Wayuda na Waisiraeli na Wayerusalemu.
20Kisha Bwana akanionyesha wafua vyuma wanne.
21Nikauliza: Hawa wanakuja kufanya nini? Akajibu kwamba: Hizo ndizo pembe zilizowatawanya Wayuda, asipatikane hata mtu mmoja aliyeweza kukiinua kichwa chake. Lakini hawa wamekuja kuzitisha na kuzibwaga zile pembe za wamizimu walioziinua pembe zao na kuzielekezea nchi ya Yuda, wapate kuwatawanya waliokuwako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.