1Bwana akasema na Mose kwamba:
2Waambie wana wa Isiraeli, warudi, wapige makambi ya kuelekea Pi-Hahiroti katikati ya Migidoli na baharini; hapo panapoelekea Baali-Sefoni ndipo, mpige makambi karibu ya baharini.
3Ndipo, Farao atakapowawazia wana wa Isiraeli kwamba: Wao wamekwisha kutatanishwa katika nchi hiyo, nayo nyika imewafungia njia, wasitoke.
4Nami nitaushupaza moyo wa Farao, ajihimize kuwafuata, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, Wamisri watambue, ya kuwa mimi ni Bwana. Basi, wakafanya hivyo.Farao anawafuata Waisirali.
5Mfalme wa Misri alipopashwa habari, ya kama wale watu wamekimbia, ndipo, moyo wake Farao, nayo mioyo ya watumishi wake ilipogeuka kuwataka tena wale watu, wakasema: Hapo tumefanya nini, tukiwapa Waisiraeli ruhusa kwenda zao na kuziacha kazi za kututumikia sisi?
6Kisha akalitengeneza gari lake, akawachukua nao watu wake kwenda naye,
7tena akachukua magari ya vita 600 yaliyochaguliwa na magari yote yaliyopatikana huko Misri, nao wakuu, aliowatia katika kila gari lake.
8Maana Bwana alikuwa ameushupaza moyo wake Farao, mfalme wa Misri, ajihimize kuwafuata wana wa Isiraeli, ijapo Waisiraeli walitoka kwa nguvu za mkono ulioko juu.Waisiraeli wanapita baharini.
15Bwana akamwambia Mose: Unanipigiaje makelele? Waambie wana wa Isiraeli, waondoke!
16Wewe nawe iinue fimbo yako na kuikunjulia bahari mkono wako, uitenge! Ndivyo, wana wa Isiraeli watakavyopita pakavu katikati ya bahari.
17Nami utaniona, nikiishupaza mioyo ya Wamisri, waingie nao na kuwafuata ninyi, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, kwa magari yake na kwao wapanda farasi wake.Wamisri wanaangamia baharini.
23Wamisri wakawafuata mbiombio, farasi wa Farao na magari yake nao walioyapanda, wote pia wakaingia nyuma yao humo katikati ya bahari.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.