1Mambo yalipokatwa, kwamba tutweke kwenda Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine mikononi mwa bwana askari, jina lake Yulio aliyekuwa wa kikosi kilichomlinda mfalme aliye mkuu peke yake.Kuokoka.
27Usiku wa kumi na nne ulipofika, nasi tulipotupwa huko na huko katika bahari ya Adiria, usiku wa manene wabaharia wakawaza kwamba: Nchi iko karibu.
28Walipokishusha kipimo, wakapaona, pana mikono 60. Walipoendelea kidogo, wakakishusha kipimo tena, wakapaona, pana mikono 45.
29Tukaogopa, tusitupwe mahali penye miamba, kwa hiyo wakatia nanga nne za nyuma, wakangoja, kuche.
30Lakini wabaharia walitaka kukimbia na kukiacha chombo. Kwa hiyo wakaishusha mashua baharini, wakasema: Twataka kuzitia hata nanga za mbele.
31Ndipo, Paulo alipomwambia bwana askari nao askari wenyewe: Hawa wasipokaa humu chomboni, ninyi hamtaweza kuokoka.
32Ndipo, askari walipozikata kamba za masha, wakaiacha, ianguke baharini.
33Kulipopambazuka, Paulo akawabembeleza wote, wale chakula, akisema: Leo ni siku ya kumi na nne, mkikaa kwa kungoja na kufunga; hakuna kitu cho chote, mlichokitia vinywani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.