1Atalia, mamake Ahazia, alipoona, ya kuwa mwanawe amekufa, akaondoka, akawaangamiza wazao wote wa kifalme.
13Atalia alipozisikia sauti za wapiga mbio na za watu, akaja naye hapo, watu walipokuwa, penye Nyumba ya Bwana.
14Alipotazama, akamwona mfalme, akisimama katika ulingo kama desturi, nao wakuu na wapiga matarumbeta wakisimama kwake mfalme, nao watu wote wa nchi yao wakawa wenye furaha na kupiga matarumbeta. Ndipo, Atalia alipoyararua mavazi yake na kupiga kelele kwamba: Mmedanganyika! Mmedanganyika!
15Ndipo, mtambikaji Yoyada alipowaagiza wakuu wa mamia waliovisimamia vikosi, akawaambia: Mtoeni hapa penye mipango ya watu! Naye atakayemfuata na auawe kwa upanga! Kwani mtambikaji alisema, asiuawe Nyumbani mwa Bwana.
16Wakamkamata kwa mikono, naye alipofika penye njia, farasi waliyoishika ya kuingia nyumbani mwa mfalme, akauawa hapo.Waisiraeli wanarudi kwake Mungu.
17Kisha Yoyada akafanya agano na Bwana, yeye na mfalme wa watu, wawe ukoo wake Bwana; agano jingine akamfanyia mfalme na watu.
18Ndipo, watu wote wa nchi hiyo walipoiingia nyumba ya Baali, wakaibomoa, nazo meza za kumtambikia na vinyago vyake wakavivunjavunja kabisa, naye Matani, mtambikaji wa Baali, wakamwua mbele ya meza za kutambikia. Kisha yule mtambikaji akaweka wakaguzi wa Nyumba ya Bwana.2 Fal. 10:26-27; Amu. 6:25.
19Kisha akawachukua wakuu wa mamia nao askari nao wapiga mbio pamoja na watu wote wa nchi hii, wakamtoa mfalme Nyumbani mwa Bwana, wakaingia nyumbani mwa mfalme na kushika njia ya lango la wapiga mbio; ndivyo, alivyopata kukaa katika kiti cha kifalme cha wafalme.
20Nao watu wote wa nchi hii wakafurahi, nao mji ukatulia. Lakini Atalia walikuwa wamemwua kwa upanga nyumbani mwa mfalme.
21Naye Yoasi alikuwa mwenye miaka saba alipoupata ufalme.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.