1Samusoni alipotelemka kwenda Timuna akaona huko Timuna mwanamke kwao vijana wa kike wa Wafilisti.
2Alipopanda kwao akamwambia baba yake na mama yake kwamba: Nimeona mwanamke huko Timuna kwao vijana wa kike wa Wafilisti, sasa mchukueni, awe mke wangu!
3Baba yake na mama yake wakamwambia: Kumbe kwetu hakuna mwanamke kwao vijana wa kike wa ndugu zako walio ukoo wetu, wewe ukienda kuchukua mwanamke kwao Wafilisti wasiotahiriwa? Lakini Samusoni akamwambia baba yake: Huyo mchukue, awe mke wangu! Kwani ndiye apendezaye machoni pangu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.