5 Mose 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Maagizo kumi ya Mungu.

1Mose akawapazia sauti Waisiraeli wote, akawaambia: Sikieni, Waisiraeli, maongozi na maamuzi, mimi ninayoyasema leo masikioni mwenu, mjifundishe na kuyaangalia, mpate kuyafanya!

2Bwana Mungu wetu alifanya Agano na sisi kule Horebu;(6-31: 2 Mose 20.)

6Mimi ndimi Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa.

7Usiwe na miungu mingine ila mimi!

16Mheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, siku zako zipate kuwa nyingi, nawe upate kuona mema katika nchi, akupayo Bwana Mungu wako!

17Usiue!

18Usizini!

19Usiibe!

20Usimshuhudie mwenzio uwongo!

21Usimtamani mke wa mwenzio!

Wala usiitamani nyumba ya mwenzio, wala shamba lake,

wala mtumishi wake wa kiume, wala wa kike,

wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote,

mwenzio alicho nacho!

22Maneno haya Bwana aliwaambia wao wote wa mkutano wenu kule mlimani kwa sauti kuu toka motoni mle winguni mwenye weusi, hakuongeza neno, kisha akayaandika katika mbao mbili za mawe, akanipa mimi.2 Mose 31:18.

23Ikawa, mlipoisikia sauti toka gizani, nao mlima ulipowaka moto, mkanikaribia ninyi mliokuwa vichwa vya mashina yenu na wazee wenu,

24mkasema: Tazama, Bwana Mungu wetu ametuonyesha utukufu na ukuu wake, tukaisikia nayo sauti yake toka motoni, siku hii ya leo tumeona, ya kuwa Bwana anasema na mtu, naye hafi.5 Mose 4:33.

25Sasa mbona tufe, moto huu mkubwa ukitula? Tukiendelea kuisikia tena sauti ya Bwana Mungu wetu hatuna budi kufa.

26Kwani yuko wapi mwingine mwenye mwili, ndiye aisikie kama sisi sauti ya Mungu Mwenye uzima, akisema toka motoni, kisha awepo mwenye uzima?

27Nenda wewe, uyasikilize yote, Bwana Mungu wetu atakayoyasema, kisha wewe tuambie yote, Bwama Mungu wetu aliyoyasema! Nasi tutakapoyasikia tutayafanya.

28Bwana alipozisikia sauti za maneno yenu, mliyoniambia, yeye Bwana akaniambia: Nimezisikia sauti za maneno ya watu hawa, waliyokuambia, hayo yote waliyoyasema ni mema.

29Laiti wangekuwa siku zote wenye mioyo inayoniogopa hivyo, wayaangalie maagizo yangu yote, wao na wana wao wapate kuona mema kale na kale!4 Mose 11:29; 5 Mose 29:4.

30Nenda, uwaambie: Rudini tu mahemani mwenu!

31Lakini wewe uje hapa kusimama kwangu, nikuambie maagizo na maongozi na maamuzi yote, utakayowafundisha, wayafanye katika nchi hiyo, mimi nitakayowapa, waichukue, iwe yao.

32Kwa hiyo angalieni, mfanye, kama Bwana Mungu wenu alivyowaagiza ninyi, msiondoke kwake kwenda wala kuumeni wala kushotoni!5 Mose 4:2; 28:14; Yos. 1:7; Fano. 4:27.

33Ila njia zote, Bwana Mungu wenu alizowaagiza ninyi, zishikeni na kuzifuata, mkae uzimani na kuona mema, nazo siku zenu ziwe nyingi katika nchi, mnayokwenda kuichukua, iwe yenu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help