Mashangilio 6 - Swahili Roehl Bible 1937

Kilio cha mtu aliyeugua mwili na moyo.(Wimbo wa juto wa 1.)Kwa mwimbishaji, wa kuimbia mazeze yenye nyuzi nane. Wimbo wa Dawidi.

1Bwana usinipatilize kwa makali yako,

4Ee Bwana, rudi, uiopoe roho yangu! Niponye kwa hivyo, ulivyo mwenye utu!

5Kwani kwao waliokwisha kufa hakuna anayekukumbuka, nako kuzimuni yuko nani atakayekushukuru?

6Kwa kupiga kite nimechoka, nikakiogesha kitanda changu usiku wote, nikayalowesha malalo yangu kwa machozi yangu.

7Macho yangu yamenyauka kwa uchungu, yakachakaa kwa ajili yao wote wanisongao.

8Ondokeni kwangu, nyote mfanyao maovu! Kwani Bwana huzisikia sauti za kilio changu.

9Bwana husikia, ninavyomlalamikia, Bwana huyapokea maombo yangu.

10Adui zangu watapatwa na soni wote kwa kustushwa sana, watarudi nyuma kwa kuingiwa na soni kwa mara moja.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help