3 Mose 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Nyama wenye kutakata na wenye uchafu.(Taz. 5 Mose 14:2-21.)

1Bwana akasema na Mose na Haroni, akawaambia:

41Nyama wadogo wanaotambaa juu ya nchi wote pia wawe tapisho kwenu, wasiliwe.

42Wote wanaojikokota tumboni nao wote wanaokwenda kwa miguu minne nao wote wenye miguu mingi zaidi, wale wadudu wote wanaotambaa juu ya nchi msiwale, kwani ndio tapisho.

43Msijifanye wenyewe kuwa tapisho kwa ajili ya hao wadudu watambaao, wala msijipatie uchafu kwa ajili yao mkichafuliwa nao.

44Kwani mimi ni Bwana, Mungu wenu, kwa hiyo sharti mjitakase, mwe watakatifu, kwani mimi ni mtakatifu. Msijipatie uchafu wenyewe kwao hao wadudu wote wanaotambaa juu ya nchi.3 Mose 19:2.

45Kwani mimi ndiye Bwana aliyewatoa ninyi katika nchi ya Misri na kuwapandisha kuja huku, niwe Mungu wenu; kwa hiyo sharti mwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu!

46Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya nyama na ya ndege na ya viumbe vyote vyenye uzima vinavyotembea majini na ya wadudu wote watambaao juu ya nchi,

47mpate kuwapambanua walio wachafu nao wanaotakata, ndio nyama wanaoliwa nao wasioliwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help