1Yosia alikuwa mwenye miaka 8 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 31 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Yedida, binti Adaya, wa Boskati.
2Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana, akaendelea na kuzishika njia zote za baba yake Dawidi, hakuziacha na kujiendea, wala kuumeni, wala kushotoni.Kitabu cha Maonyo kinaoneka.
8Ndipo, mtambikaji mkuu Hilkia alipomwambia mwandishi Safani: Nimeona kitabu cha Maonyo Nyumbani mwa Bwana. Kisha Hilkia akampa Safani hicho kitabu, akakisoma.
9Mwandishi Safani akaja kwa mfalme, akampasha mfalme habari na kumwambia: watumishi wako wamezimimina fedha zilizoonekana Nyumbani mwa Bwana, wakazitia mikononi mwao wenye kazi waliowekwa kuisimamia Nyumba ya Bwana.
10Kisha mwandishi Safani akamsimulia mfalme kwamba: Mtambikaji Hilkia amenipa kitabu; kisha Safani akakisoma mbele ya mfalme.
11Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya kitabu cha maonyo, akazirarua nguo zake.
12Kisha mfalme akamwagiza mtambikaji Hilkia na Ahikamu, mwana wa Safani, na Akibori, mwana wa Mikaya, na mwandishi Safani na Asaya aliyekuwa mtumishi wa mfalme kwamba:
13Nendeni kuniulizia Bwana mimi na ukoo huu na Wayuda wote kwa ajili ya maneno ya hiki kitabu kilichooneka! Kwani makali ya Bwana yenye moto ni makuu, nayo yanatuwakia sisi, kwa kuwa baba zetu hawakuyasikia maneno ya kitabu hiki na kuyafanya yote, tuliyoandikiwa humo.
Mfumbuaji wa kike Hulda.14Ndipo, mtambikaji Hilkia na Ahikamu na Akibori na Safani na Asaya walipokwenda kwa mfumbuaji wa kike Hulda, mkewe Salumu, mwana wa Tikwa, mwana wa Harihasi aliyeyaangalia mavazi; naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili, wakasema naye.
15Akawaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mwambieni yule mtu aliyewatuma kwangu:
16Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikileta mabaya makali hapa, yawapate wenyeji wa hapa, ndiyo yote, kile kitabu kinayoyasema, alichokisoma mfalme wa Wayuda,
17Kwa kuwa wameniacha, wakavukizia miungu mingine, wanikasirishe kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo makali yangu yenye moto yatapawakia mahali hapa, nayo hayatazimika.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.